Pages

Saturday, November 10, 2012

LORD EYES NA MENEJA WAKE WAKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

Msanii Lord Eyes na mwanasheria wake Peter Kibatala wakiwa Double View ambapo walizungumza na waandishi wa habari
Msemaji wa kundi la WEUSI Nikki wa Pili,Mwanasheria,Lord Eyes na G Warawara
Mwanasheria akitoa ufafanuzi
Wakili wa Lord Eyes leo ametoa ufanunuzi kuhusu tukio lililotokea la msanii huyo kuhusishwa na wizi wa vifaa vya kwenye gari.
 
Wakili huyo alisema kua dhumuni la kuwaita waandishi wa habari leo ni kutaka Jamii itoe nafasi kwa vyombo vya sheria kutoa majibu juu ya tuhuma hizo baada ya hapo ndo waanze kuongea.
 
Sahivi kinachoendelea ni habari ambazo watu hawana uhakika nazo.
 
Wakili huyo alisema kuwa Lord Eyes hana hatia hadi pale vyombo vya sheria vitakaposema kuwa msanii huyo kweli anahusika na shutuma hizo za uwizi.
 
Kwa upande wa Lord Eyes amesema kuwa watu wanajua kuwa yeye ni mwanamuziki kwa muda wote na hajihusishi na maswala ya uwizi na ameomba mashabiki wavumilie kipindi hichi ambacho anapigania haki na ukweli utajulikana.
 

0 maoni:

Post a Comment

Labels