Pages

Friday, November 09, 2012

TMK FAMILY KUACHIA NGOMA MPYA IITWAYO "TUTAONEKANAJE"



 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Na Elizabeth John
KUNDI la wakongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini, ‘TMK wanaume Family’ wanajipanga kuachia kibao chao kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Tutaonekanaje’ ambacho wanatarajia kukiachia Novemba 17 mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Said Juma ‘Chege’ ambaye ni mmoja wa kundi hilo, alisema ni muda mrefu hawajatoa wimbo wa pamoja hivyo wameamua kufanya hivyo ili kuwapa raha mashabiki na wapenzi wao.

Alisema wimbo huo utafanya vizuri sokoni kutokana na ujumbe uliopo ndani yake na kwamba utakua ni pamoja na video yake.

“Inapendeza unapotoa audio iwe inakuja pamoja na video yake kwa lengo la kuwapa burudani iliyotulia mashabiki wako na .inapokuja peke yake inakua haina burudani kwa wadau, video ndio mpango mzima,” alisema Chege.

Mbali na kutaka kutoka na kibao hicho, Wanaume Family walishawahi tamba na vibao vingi kikiwemo cha ‘Kichwa kinauma’ ambacho kilifanya vizuri na kutikisa tasnia ya muziki wa bongo fleva.

0 maoni:

Post a Comment

Labels