Pages

Tuesday, November 13, 2012

BEN PAUL KUTOA TRUCK NA WALTER CHILAMBO

Na Elizabeth John

MKALI wa muziki wa RnB nchini, Benard Paul ‘Ben Pol’ amesema kwa kiwango alichokionesha mshindi wa Epiq Bongo Star Search 2012, Walter Chilambo, ameamua kufanya nae kazi pamoja na kumshirikisha baadhi ya kazi zake.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ben Pol alisema hakujua kama kuna watanzania ambao wanatamani kazi anazozifanya na wanaotamani kuwa kama yeye wakati bado ni mchanga katika fani hiyo.

“Kwangu naona ni heshima kubwa sana msanii chipukizi kuimba wimbo wangu na kuutendea haki jukwaani kama kautunga yeye, nafurahi kuona mashabiki wananikubali katika kazi zangu,” alisema Ben Pol.

Alisema kwasasa yupo kwenye mchakato wa kuachia video ya wimbo wake mpya wa ‘Pete’ ambao unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Mkali huyo ambaye aliwahi kutwaa tuzo ya mwanamuziki bora wa RnB mwaka jana na mwaka huu kwa kupitia nyimbo zake za ‘Nikikupata’ na ‘Number one Fun’, anawaomba wadau wa muziki huo kuendelea kumpa sapoti Walter pale anapohitaji msaada kutoka kwao.
 

0 maoni:

Post a Comment

Labels