Pages

Tuesday, November 13, 2012

MB DOGG APANIA KUTOKA NA 'AMENIMISS'


Na Elizabeth John

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Mb Doggy anajipanga kuachia kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Amenimiss’ baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu.

Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Mb Doggy amesema yupo katika hatua za mwisho za uaandaaji wa kibao hicho ambacho kitakua na ujumbe mzito kwa jamii pamoja na wapenzi wa kazi zake.

“Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu nimeamua kutoka na kibao hicho ambacho naamini kitakua moto wa kuotea mbali kwa mashabiki wangu kutokana na ubora wa kazi yenyewe,” amesema Mb Doggy.

Amesema anaomba mashabiki wake wakae mkao wa kula kwaajili ya kukipokea kibao hicho ambapo kwa sasa yupo kwenye hatua za mwisho za uandaaji wa video ya ngoma hiyo.

Mbali na kibao hicho, Mb Doggy alishawahi kutamba na vibao vyake kama, Si Uliniambia, Inamaana na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa bongo fleva.
 

0 maoni:

Post a Comment

Labels