Pages

Tuesday, November 13, 2012

MSANII WA TAARABU ALIYEFARIKI DUNIA

Msanii wa Taarabu Mariam Khamisi aliyekuwa akiimba TOT  mwenye Tisheti nyekundu pichani ndiye aliyefariki dunia wakati akijifungua katika hospitali ya Muhimbili.

Msanii wa muziki wa taarab nchini Tanzania wa kundi la Tanzania One Threter TOT, Mariam Khamis maarufu kama paka mapepe amefariki dunuia usiku wa jana kuamkia leo katikam hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa baba mzazi wa marehemu Khamis Muhidini Shomary Maria Khamisi alifariki kwa kifo cha uzazi mara baada ya kujifungua hospitalini hapo.

Mariam enzi za uhai wake aliwahi kuimbia katika makundi mbalimbali ya muziki wa taarab likiwamo East Africa Meldy ambapo alirikodi kibao kilichomfanya kulikana kilichokwenda kwa jina PAKA MAPEPE, makundi mengine ni Zanzibar Stars ambapo alidumu kwa muda mrefu huku akitamba na vibao kama Narindima naye, Raha ya Mapenzi na nyinginezo.

Alipokuwa 5stars mariam alitamba na nyimbo kama Ndo Basi tena, Uzushi hauniitii Doa na baadaye aliamua kuhama katika kundi hilo na kwenda TOT ambapo alirekodi kibao kilichikwenda kwa jina la SIDHULIKI NA LAWAMA, na alidumu hapo mpaka umauti ulipomfika.

Mipango ya mazishi inaendelea kufanyika ambapo anatarajiwa kuzikwa kesho Magomeni Kota jijini Dar es Salaam. 

Pole kwa marafiki,ndugu na wapenzi wa muziki wa Taarab nchini

MUNGU AIPUMZISHE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI..AMENI 

0 maoni:

Post a Comment

Labels