Pages

Friday, November 09, 2012

KUNDI LA TOP FLEVA KESHO KUZINDULIWA

 
Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Barnaba Elias, kesho anatarajia kulizindua kundi jipya la muziki wa kizazi kipya la Top Fleva, katika onesho maalumu litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Kakala Kigamboni, Dar es Salaam.

Uzinduzi huo wa kundi, utaambatana na uzinduzi wa studio yao mpya inayokwenda kwa jina la Shebi's Records ambayo lengo lake ni kuibua wasanii chipukizi.

Akizungumza Dar es Salaam jana Barnaba, alisema kuwa anatarajia kufanya onyesho la aina yake kwa ajili ya kulitambulisha kundi hilo jipya.

Alisema kuwa atatumia fursa hiyo kuimba nyimbo mbalimbali ikiwa ni pamoja na zile za zamani ili kutoa burudani safi kwa mashabiki na wapenzi wa muziki huo.

"Ninatarajia kufanya onesho la aina yake kwa ajili ya kulitambulisha rasmi kundi jipya la muziki wa kizazi kipya ambapo lina lengo la kuleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya muziki" alisema.

Naye Mkurugenzi wa kundi hilo Shaban Ramadhan alisema kuwa wanatarajia kutua na Helcopta katika Uwanja wa Machava ulipo Kigamboni kabla ya kuingia ukumbini.

Alisema kuwa kundi lao ni jipya ambapo lina jumla ya wasanii watatu ambao ni pamoja na Salum Shaban 'Manginja', Tabisa Stanley 'Tista' na Tonel Emilian 'Ton Touch'.

Alisema kuwa mpaka sasa wameshakamilisha jumla ya nyimbo tatu ambazo ni Top Fleva, Comlete waliyomshirikisha Ney wa Mitego pamoja na Uchumi Unayumba ambayo wamemshirikisha Chege.


0 maoni:

Post a Comment

Labels