Pages

Friday, November 09, 2012

MAMBO AMBAYO WASANII WACHANGA YANAWAFANYA WASITOKE HARAKA KATIKA MUZIKI

 i;-Wasanii wachanga kutoenda na wakati(MUDA).
Unakuta wasanii wakubwa kama watano nao wanakazi mpya ambazo wanahitaji kuziachia katika vituo mbalimbali vya Redio na msanii chipukizi nae anatakakuachia kazi yake je, unafikiri huyu msanii anayechipukia anaweza kupata airtime kama wasanii walitoka tayari katika mziki,kwa msanii unaechipukia inatakiwa uende na muda iliuweze fanikiwa.

ii;-Rushwa
Kuna Baadhi ya watangazaji ambao wameweka kama sehemu ya kujipatia kipato au kudai fedha pindi wasanii wachanga wanapokuwa wanahitaji kazi zao kupewa airtime kama wasanii wakubwa au wenye majina.

Hii inaweza ikamfanya msanii mchanga ambaye hana fedha kufail katika game la muziki na hili pia naona Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ihusike kwani nimoja kati ya Rushwa.

iii;-Nidham Mbovu kwa wasanii chipukizi,
Muda mwingine wasanii hawa wanaochipukia wanaweza kujipoteza wenyewe katika game kutokana na Dharau au kujiona wamesha toka kimuziki hii inatokana na wao kutoa ngoma ambayo labda imepata airtime katika Redio kubwa na imehit mwisho wasiku huleta dharau kwa mafuns wao na kujiona yeye ni superstar.

0 maoni:

Post a Comment

Labels