Pages

Tuesday, December 04, 2012

Kim Kardashian ndiye mrembo aliyetafutwa zaidi kwenye yahoo! Mwaka 2012, Mikasa ya mapenzi yampandisha.



Mwanamitindo Kim Kardashian amefunika kwenye top ten ya 2012 Yahoo! Searched list. Nyota ya mrembo huyo imeng’aa na kumuweka nafasi ya juu akiwafunika watu wengine maarufu na warembo wenye majina makubwa.

Jina la the Kanye West’s chocolate limeshika nafasi ya tatu baada ya nafasi ya kwanza kukamatwa na ‘election’ na nafasi ya pili kwenda kwa “iPhone 5”. Hii inamfanya Kim kuwa ndiye the most searched person katika kipindi cha mwaka 2012. 

Kwa mujibu wa Vera Chan, ambae ni mchambuzi wa Yahoo! Web trend, Kardashian alitafutwa zaidi kwa sababu ya umarufu uliotokana na matukio yake na mikasa ya mapenzi. 
 
Moja kati ya mikasa iliyowashawishi watu kumtafuta zaidi kwenye Yahoo! ni battle kati yake na mmewe wa zamani Kris Humphries, na iliyompandisha zaidi ni mikasa kibao ya kimapenzi kati yake na rapper Kanye West.

Sio hayo tu, Vera Chan alisema reality series yake inayorushwa kupitia television ya E! Iliwapa sababu watu wengi ku-msearch kwenye Yahoo!

Mchambuzi huyo amesema,kitu cha kushangaza katika nomination zilizoleta list ya top ten ya mwaka huu ni kwamba habari zote zilizoingia kwenye website zilikuwa zimesomwa tayari na watu, lakini watu waliendelea kuzi-search tena habari hizo hizo mwaka mzima.

Katika list hiyo Kardashian amewafunika wanawake maarufu wengine kama Whitney Houston ambae kifo chake mwaka huu kilisababisha watu wengi wazitafute habari zake, Lindsay Lohan na Jenifer Lopez ambae alikuwa judge wa ‘American Idol’.

Hii ndiyo top 10 ya watu na vitu vilivyotafutwa kupitia Yahoo! mwaka 2012
1.            Election
2.            iPhone 5
3.            Kim Kardashian
4.            Kate Upton
5.            Kate Middleton
6.            Whitney Houston
7.            Olympics
8.            Political polls
9.            Lindsay Lohan
10.         Jennifer Lopez

0 maoni:

Post a Comment

Labels