Pages

Friday, December 28, 2012

Top 20 ya wasanii waliojitolea zaidi kusaidia jamii mwaka 2012...Taylor Swift aongoza, list yamtema Rihanna.


Taylor Swift
Japokuwa jamii ndiyo inayomuweka juu mtu yeyote lakini pia hutegemea kitu kutoka kwake baadae kulingana na moyo wake mwenyewe na anavyoiona jamii ya wahitaji mbalimbali, kwa kujitolea kuisaidia jamii hiyo tunaita 'kuirudishia jamii" ama kwa lugha ya kigeni tunaweza kusema 'giving back to the society'

Kwa mujibu wa mtandao wa shirika la kusaidia jamii "DoSomething.org.' mwaka 2012 mwimbaji wa kike wa Pop na Country Taylor Swift ndiye ameshika nafasi ya kwanza akifatiwa na mwimbaji mkongwe wa pop na rock Miley Cyrus.


Taylor Swift alitumia mkwanja mrefu sana kwa ajili ya kutoa misaada ya kibinadamu kwa mwaka 2012 kiasi cha $ 4million, kiasi ambacho hakikufikiwa na celeb yeyote.

Miley Cyrus aliyeshika nafasi ya pili yeye aliitumikia jamii zaidi kwa kusaidi kuelimisha watu wengi zaidi kuhusu utunzaji wa wanyama, lakini pia sapoti yake katika kuinua muziki kupitia kampeni ya "Save The Music Foundation" na "Make-A-Wish Foundation", na hizi ni baadhi tu.

Celebs wengine ambao wameingia kwenye list hiyo ni Lady Gaga, Justin Bieber, Selena Gomez, Demi Lovato, Carrie Underwood, Sofia Vergara, Beyonce Knowles, Jay-Z, Ian Somerhalder, Pink, Ben Afleck na wengine wengi.

Jay Z & Beyonce
Lady Gaga
Unfortunately, Rihanna ambae mwaka huu umekuwa mwaka wake wa mafanikio sana, kiasi cha kuingia kwa mara ya kwanza kwenye Billboard Chat Top 200 na album yake ya 'Unapologetic', na kununua jumba la kifahari la dola million 12. Hata hivyo haimaanishi kuwa hatoi misaada, hata hivi karibuni aliisaidia sana hospitali ya kwao Barbados kiasi cha dola million 1.75 ili kuanzisha kitengo maalum cha kansa.
Justin Bieber
 
Hii ndio list ya top 20 ya celebs waliojitolea zaidi kusaidia jamii:

1. Taylor Swift
2. Miley Cyrus
3. Channing Tatum
4. Lady GaGa
5. Justin Bieber
6. Robin Roberts
7. Pink
8. LeBron James
9. Selena Gomez
10. Ian Somerhalder
11. Jay-Z & Beyonce Knowles
12. George Takei
13. Ben Affleck
14. Andrew Garfield & Emma Stone
15. Ryan Seacrest
16. Demi Lovato
17. Carrie Underwood
18. Olivia Munn
19. Sofia Vergara
20. Drew Brees

0 maoni:

Post a Comment

Labels