Pages

Sunday, December 16, 2012

UKWELI KUHUSU GANGWE MOBB ,MUZIKI NA NDOA YA INSPECTOR HAROUN.

Mkongwa wa muziki wa Bongo Fleva kupitia Rap Katuni, Inspector Haroun amefunguka kuhusu mambo tofauti kwenye maisha yake Ikiwemo ndoa yake. 

Inspector amesema haja tengana na mke wake na mapenzi yao yana nguvu kama kawaida,Hata suti aliyo vaa hapo kwenye picha alitayarishiwa na mke wake. 

Inspector amenukuliwa  akisema yameongelewa mengi kuhusu ndoa yake kuvunjika kwenye mitandao na radio tofauti lakini stori zote hizo hazina ukweli.

Inspector Haroun Na Sammisago
Kuhusu mahusiano yake na Luteni Kalama wa Gangwe Mobb, Inspector ameweka wazi kuwa hawana beef na kila siku wana wasiliana na kuongea mambo tofauti kuhusu mziki na maisha. 

Napenda ufahamu kuwa kwa zaidi ya miaka 3 Inspector hajafanya wimbo mkubwa uliomuweka juu kama nyimbo zake za awali na kwa sasa anampango wakufanya hivyo kwenye wimbo wake mpya. 

Inspector Haroun yupo studio na Dully Sykes wakitengeneza wimbo mpya utakao toka na video yake kwa pamoja.

0 maoni:

Post a Comment

Labels