RAY C akimshukuru Rais Kikwete kwa matibabu Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C watu kushoto,Mama yake
mzazi RayC Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada
yake Ray C. (picha na Freddy Maro).
Msanii wa Kizazi Kipya hapa nchini ,maarufu kama Bongo Flavour, Bi Rehema Chalamila anaejulikana zaidi kama Ray C,
leo mchana amefika Ikulu ya Dar-Es-Salaam kumshukuru Rais Jakaya Mrisho
Kikwete kwa msaada mkubwa wa matibabu yake ambayo yanafanyika jijini
Dar-Es-Salaam chini ya uangalizi maalum
Ray C
amefika Ikulu akiongozana na mama yake mzazi Bibi Margareth Mtweve
ambaye pia amemshukuru Rais Kikwete kwa msaada huo mkubwa ambao
umesaidia kurudisha hali ya kawaida ya Ray C.
Rais amempongeza Ray C kwa kukubali hali yake ya kiafya na hatimaye kukubali kupata matibabu ambayo bado anaendelea nayo chini ya uangalizi maalum.
Rais
amemtaka mwanamuziki huyo kufuata masharti ya madaktari ili aweze kupona
kabisa na hatimaye kurudia hali yake ya mwanzo na kurejea katika
shughuli zake za kujitafutia kipato na maisha.
Kwa vile Ray C
bado yuko katika matibabu, hatutaweka wazi sehemu anayotibiwa hadi
atakapokuwa tayari kabisa kurudi katika shughuli zake rasmi hivyo
tunaomba jamii impe ushirikiano huo na kuheshimu taratibu zake za
matibabu ili hatimaye aweze kupona kikamilifu.
“MWISHO”
Imetolewa na :
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu-DSM
10 Desemba, 2012
0 maoni:
Post a Comment