Mbunge wa viti maalum (CCM) Ritta Kabati akiingiza mashairi
katika wimbo mpya akishirikiana na vijana chupikizi 20 wa kabati star
search katika studio za Top Magic Sound zilizoko Ipogoro Iringa mjini.
Na Denis Mlowe – Iringa
Muziki
wa kizazi kipya wengi wanaujua kama bongo fleva
wazidi kuwavutia viongozi mbalimbali na wengine wanaimba hadi sasa kama
Joseph Mbilinyi aka Sugu, Vick Kamata sasa amejitokeza mbunge mwengine
wa viti maalum toka chama cha mapinduzi Ritta Kabati na kuufanya uwe
gumzo katika maisha ya
watanzania na nchi za jirani kitu kinachofanya watu mbalimbali
kujitokeza
kuupenda na wengine kuamua kuingia kwa kasi katika tasnia hii ya
burudani Tanzania.
Katika
kuukuza zaidi muziki huu Mbunge wa Viti maalum kupita
chama cha Mapinduzi mkoani Iringa Ritta Kabati akishirikiana na wasanii
chipukizi 20 wa kwanza waliotokana na shindano la kutafuta vipaji la
Kabati
Katiba Star Search amefanikiwa kutoka wimbo mmoja unaokwenda kwa jina la
'Iringa Bila Ukimwi Inawezakana' uliofanywa katika studio za Top Magic
Sound chini ya
mzalishaji anayekuja kwa kasi pande za Nyanda za juu Kusini Ecko Msigwa.
Wimbo huo ni harakati za mbunge Kabati alizozianzisha katika
kuwakomboa vijana katika majanga kama uvutaji wa bangi, kuepukana na maambukizi
ya ukimwi katika mkoa huu ambao unaongoza kwa sasa nchini Tanzania na amesema
kwamba wakati anafikiria kuingiza mashairi hayo kwa kweli alikuwa katika hali
ya huzini kwa jinsi vijana walivyoweza kufanya vizuri katika wimbo huo kwa
lengo la kuwakomboa watanzania kupitia muziki.
Baadhi ya mashairi ya hayo ni ‘ndugu zangu watanzania nina
maumivu makali sana, tumepoteza ndugu zetu, jamaa zetu na marafiki zetu dira ya
maendeleo inateketea ni wakati wetu kupambana iringa bila ukimwi inawezekana’ “
kwa kweli nina uhakika wa kuwafunika vijana hawa katika wimbo huu ambao
unasubiriwa kwa hamu kubwa na wakazi wa mkoa huu kwa kuwa ni mkusanyiko wa
vipaji vya kweli vilivyotokana na shindano nililoandaa” alisema Kabati
Wimbo huo unatarajia kuzinduliwa rasmi leo katika radio zote
za Nyanda za Juu Kusini na kisha kusambazwa katika radio zote nchini Tanzania na
amewataka wadau kuwapa nguvu vipaji hivi kwa kununua kazi za vijana kwa lengo
la kuwaongeza kipato na kuondoka na maisha ya vijiweni.
0 maoni:
Post a Comment