Pages

Thursday, December 20, 2012

Rihanna Anunua Jumba La Kifahari Linalogharimu Kiasi Cha $12 Million Za Kimarekani...

       
Superstar kutoka nchini Marekani, ambae anafanya kazi na kupata mafanikio makubwa kupitia kazi yake ya muziki, Rihanna, sasa amenunua nyumba yake mwenyewe ambapo nyumba hiyo inakadiriwa kumgharimu mwanadada huyo kiasi cha dola za kimarekani 12 milioni katika mji wa Pacific Palisades, California. 

Nyumba hiyo ambayo ina ukubwa wa square feet 11,000 ambayo ina vyumba saba, mabafu pamoja na vyoo tisa, jiko, sehemu ya kulia chakula na pia ina sehemu ya kuchomea nyama kwa nje pamoja na bar. Nyumba hiyo, pia ina bwawa la kuogelea kubwa lenye urembo wa kisasa. 

Pia jumba hilo lina sehemu kubwa tu ya kuweza kuhifadhi magari hadi kufikia 20. 

Rihanna pia alisema kupitia ukurasa wake wa twitter kuwa huwa anaamka kila siku asubuhi ya saa kumi na moja alfajiri na kukaa kwenye swimming pool yake hadi jua la asubuhi linapochomoza...

Tazama baadhi ya picha za jumba lake hilo la kifahali linavyoonekana:

0 maoni:

Post a Comment

Labels