Pages

Thursday, December 06, 2012

ALICHO KISEMA PROFESA JAY KUHUSU DIAMOND PLATNUMZ



 Profesa Jay a.k.a Wa Mitulinga, mmoja wa rappers wanaofanya hip-hop bongo kwa muda mrefu sana, akiwa kama waanzilishi kwa kipindi hicho akiwa na Kundi la Hard Blasters, masaa machache yaliyopita ameongea kitu kuhusu msanii mwenzie, Diamond Platnumz. 

Nikimzungumzia Platnumz , ni mwanamuziki wa Bongo Fleva amabe anafanya vizuri kwa sasa na ametokea kujijengea jina kubwa na kujikusanyia fans wengi sana katika muziki wake anaofanya....
  
Sasa, Profesa Jay, kupitia ukurasa wake wa twitter, amewaambia watu ambao wanadhani na kuwa wakisema huu ndo mwisho wa mwanamuziki huyo, yeye anaona "Dogo", kama alivyomuita kuwa bado anafanya vizuri sana na kuwaambia followers wake kuwa, kama amekuwa anakosea basi arekebishwe ili aweze kusonga... 

watu wengi wamekuwa wakizungumzia mafanikio ya Diamond Platnumz na wengine wakimzungumzia vibaya na katika kuonekana wakichukia maendeleo yake...

Ni vizuri kumsahuri mtu anaekosea ili aweze kufanya vizuri na kuendelea vyema... Check hapa chini, words from "The Heavy Weight MC" himself:


0 maoni:

Post a Comment

Labels