Pages

Friday, December 14, 2012

POLISI WANAFUATILIA VITISHO VYA MAUAJI YA RAPPER ROZAY VINAVYO FANYWA NA KUNDI LA GANGSTER DISCIPLES

 Rapper Rick Ross ambae siku za karibuni iliripotiwa kutaka kuuawa na members wa kikundi cha Gangster Disciples (GDs) chenye maskani yake huko Chicago ambacho kilituma video kikimtaka MMG Boss kumlipa mwanzilishi wa kikundi hicho, Larry Hoover. 

Video hiyo ilisambaa sana na sasa polisi wa Chicago, yaani Chicago PD imeanza kufuatilia na kufanya uchunguzi kuhusiana na vitisho hivyo.
  
Lakini hii ikionekana kama imesababisha Ricky kusitisha shows zingine ambazo zipo katika ziara yake inayoendelea, kupitia redio moja huko Miami, Ross mwenyewe alikataa hilo na kusema kuwa yeye hawaogopi GDs ila ilibidi ahairishe shows hizo kutokana na matangazo hafifu yaliyofanywa huko na haihusiani na vitisho hivyo vya GDs na kuongeza kuwa yeye ni boss na huwezi kuahirisha show ya boss bila ruhusa ya boss mwenyewe.

0 maoni:

Post a Comment

Labels