Pages

Friday, December 14, 2012

Hatimaye Mase aondoka Bad Boy, afafanua kwanini deal yake na G-unit ilizuiliwa.



Wengi wetu tunaweza tukawa tunaamini kuwa mtu mzima Diddy na Mase walishamalizana miaka kadhaa iliyopita…lakini ukweli umefafanuliwa na Mase mwenyewe kuwa ni hivi juzi tu ndo amepata nafasi ya kuachana na Bad Boy baada ya miaka 16 na kuongeza kuwa yuko karibu ku-sign na lebel nyingine muda si mrefu.

“Nimekuwa ndani ya mkataba ule kwa miaka 16 na hatimaye sasa ameniruhusu kuondoka..big shout’out to Diddy….nadhani aliamka akijisikia vizuri na akataka kufanya kitu kizuri pia”…amesema Mase.

“Kwa sasa sitaki kuwa chini ya mtu ambaye atanifunga kwa muda mrefu sana…ni kama unapovunja uhusiano na hutaki kuingia kwenye uhusiano mwingine kwa haraka”..ameongeza.

Pia Mase ameongelea vitu vingi positive kuhusu Diddy na kusema miaka michache iliyopita Diddy alizuia yeye kwenda G-Unit kwa sababu alihitaji pesa nyingi sana na kumalizia kusema…”si unamjua Diddy alivyo..??nampenda lakini inahitaji ukate mkono wako ili akuache uondoke”.

0 maoni:

Post a Comment

Labels