Pages

Wednesday, December 12, 2012

Beyonce ampa Ne-Yo kazi ya kumuandikia nyimbo kwenye album yake, “we will get another Irreplaceable”

Beyonce

Beyonce ampa Ne-Yo kazi ya kumuandikia nyimbo kwenye album yake, “we will get another Irreplaceable”

Beyonce Knowles anazidi kuonesha utofauti katika game kwa kuhakikisha anapata kitu anachoweza kukiita kimetoka kwa “best of the best” kwa mwaka ujao ambapo amehakikisha anawapa kazi watu wenye vipaji maalum ambao wanaweza kuifanya album yake kuwa the best album from the Diva herself.

Ne-Yo
Beyonce ameamua kumshirikisha mwimbaji na mwandishi wa muziki Ne-Yo katika kuiandaa album yake inayotarajiwa kuachiwa rasmi mwaka kesho, Ne-Yo ana kazi ya kuandika wimbo utakaoimbwa na Beyonce kama alivyofanya mwaka 2006 alipoandika ‘Irreplaceable’.

Ingawa Ne-Yo anamzigo mkubwa wa project yake bado amefurahia sana kushirikishwa kwenye project ya Beyonce Knowles. 
 
Ne-Yo alionesha furaha yake wakati anaongea na MTV na akasema watu wategemee kitu kikubwa kama ‘Irreplaceable’ na kwamba anataka kuwapa fans kitu walichokuwa wanakisubiri kwa miaka sita. 
 
“Who knows? Labda tutapata Irreplaceable nyingine kwenye chat. Huwezi jua.”

Beyonce anatarajia kuachia album yake ya tano mapema mwakani na atawashirikisha wasanii wakongwe na wakali kama hubby wake Jay-Z, Miguel, The Dream, na Kanye West. 
 
Tarehe maalum ya kuachiwa album hiyo bado haijawekwa wazi lakini wimbo wa kwanza unatarajiwa kuachiwa kabla ya February.

Ne-Yo ataungana na The Dream katika kumsaidia Beyonce kuandaa album yake hiyo.

0 maoni:

Post a Comment

Labels