Pages

Friday, December 28, 2012

Hizi Ndio Sababu Zinazolifanya Kundi La P-Unit Lisivunjike

       
Kundi la P-Unit kutokea nchini Kenya ambalo lionaundwa na wasanii watatu yaani Frasha, Gabu na Bon Eye limeweza kutoa sababu ya wao kutotengana au kuwa pamoja hadi leo. 

Akiongea kwa niaba ya kundi zima la P-Unit, Gabu amesema kuwa P-Unit ni kama familia na wanaheshimiana sana, na sababu kubwa inayo wafanya waendelee kuwa na umoja katika kundi hilo ni mipango thabiti ambayo wamejiwekea, wanatambua tofauti kati ya kazi na urafiki. 

P-Unit kwasasa wanatamba na ngoma yao mpya ya You Guy ambayo wamemshirikisha Collo.

0 maoni:

Post a Comment

Labels