Pages

Thursday, December 20, 2012

Lady Jaydee Kutoa Neno Lake Tarehe 31...



Hii imekuwa kawaida haswa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka, wengi wamekuwa wakisema kitu tukiwa katika mwezi wa mwisho wa mwaka na kipindi hiki cha sikukuu, wengine hushukuru kwa kumaliza mwaka salama, wengine hushukuru kwa kufikia malengo yao n.k. 
 
Hii imekuwa tofauti kwa Binti Machozi a.k.a Binti Komando ambae yeye ametangaza kutoa neno lake siku ya mwisho kabisa ya mwaka... Yeah Tarehe 31 December!! Lady Jaydee aliyasema haya kupitia ukurasa wake wa twitter masaa kadhaa yaliyopita!
 
 Jaydee ambae ni mwimbaji, mmiliki na kiongozi wa Machozi Band aliyasema hayo na kuongeza kuwa anafahamu kuwa NENO lake litawaumiza baadhi ya watu ila yeye hatajali hilo bali anasimama upande wake na msimamo wake.... 

Sasa swali ni je?? Ni NENO gani hili?? Je Binti Komando atamuumiza nani na NENO lake hili?? Inabidi watu wajipange, maana Jaydee yuko tayari kimpango wake...

0 maoni:

Post a Comment

Labels