Albam ya tano ya rapper wa West Coast Jayceon Taylor aka The Game
iitwayo ‘Jesus Piece’ imeingia sokoni wiki hii na kusababisha hasira
kubwa miongoni mwa waumini wa dini ya kikristu kutokana na kutumia alama
zinazoikosea heshima dini hiyo.
Kava la albam hiyo lina picha ya Yesu mweusi akiwa amejifunika usoni
bandana nyekundu na cheni yenye sura ya Yesu miongoni mwa alama zingine.
Mratibu wa mawasiliano wa shirika la Save Africa’s Children Tilla
Amin Tanyi ameiambia website ya FoxNews kuwa The Game amemuonesha Yesu
kama mtu wa kawaida anayetafuta mali za dunia na kushiriki kwenye
vitendo vya kihalifu.
Albam hiyo ina nyimbo kadhaa zenye mashairi ya dini zikiwemo Heaven’s Arm na Pray.
Mwezi October mwaka huu alipolitambulisha kava la albam yake kwenye
mtandao wa Instagram inadaiwa kuwa uongozi wa kanisa katoliki uliipigia
simu label yake ya Interscope kutoa malalamiko yake.
Hata hivyo The Game anasema ameiitwa albam yake Jesus Piece kwasababu
mwezi August alibatizwa na amekuwa akienda kanisani lakini hajaacha
maisha yake ya kwenda club, kuvuta na kunywa
0 maoni:
Post a Comment