Pages

Friday, December 14, 2012

Stereo Asaini Mkataba Mpya Na Unity Entertainment

 Msanii wa miondoko ya kizazi kipya, James Minara (pichani) akijulikana vyema kisanii kwa jina la Stereo amesaini mkataba mpya na kampuni ya Unity Entertainment ambayo inafanya kazi ya kusimamia wasanii wa muziki hapa nchini Tanzania.

 Stereo anaetamba na ngoma zake kadhaa redioni, kama Nitabaki, Karibu na nyinginezo alidondoka wino huo majira ya saa 2 usiku wa jana.

Kwa mujibu wa Manager wa kampuni hiyo, Bw. Arthur, Unity EntertainmentStereo ambae kabla alikuwa anafanya kazi na M-Lab, lakini kuanzia sasa itamsimamia msanii huyo katika kazi zake zote za kisanii ikiwemo ku-record audio, kufanya videos, kuandaa matamasha, kumtangaza na vinginevyo.

imem-sign Kampuni hiyo ambayo mpaka sasa inasimamia kazi za wasanii wengine wakubwa kama AY, MwanaFA, na Fezza Kessy imemuongeza msanii huyo mara baada ya kuona kipaji chake na pia wanaweza kufanya kazi pamoja kupitia maelewano yao, na baada ya mkataba huo kazi zinaanza mara moja.

0 maoni:

Post a Comment

Labels