Warawara alifunguka katika interview aliyofanya hivi
karibuni na Josefly mtangazaji wa radio Victoria Fm ya Musoma kuwa moja kati ya
malengo yake yaliyokamilika ni pamoja na kufanya video yake ya take off,
kuachia ngoma ya bado Ngware ambayo ilitoka remix yake pia, na hivi karibuni
ameachia Mama yeyo.
Lakini akasema huwezi jua anaweza kuachia audio ya wimbo
wake aliofanya na AY ‘Take off’ ambao kwa sasa una video tu, na ikawa kama
zawadi kwa fans wake ya kufunga mwaka, “You ‘ll never know” ndicho alichosema.
G-warawara aliendelea kufunguka kuwa hayo yasingekuwa
malengo yake kama alivyotaka iwe, “kubwa nachotaka ni muziki wangu ufike nje,
kupata more shows nje na kuendelea kuwalisha watu wangu madini kadri
inavyotakiwa,” that’s G-Nako.
Na kuhusu mipango yake ya mwakani, alisema kikubwa ni
kujenga fan base yake iwe kubwa zaidi ikiwa ni pamoja na kuwaweka fans wake
pamoja, na ukishajenga fan base kubwa ndo mambo mengine yanaanzia hapo, na
Mnako huyo hajali itachukua muda gani kuikamilisha.
On top of that, G-Nako aliulizwa kwa nini Bou Nako ambae ni
member wa Nako 2 Nako hakuingia kwenye list ya majina ya kampuni ya WEUSI, na
hapo akafunguka, “unajua swala la kampuni ni swala ambalo liko tofauti kidogo
na ni swala ambalo liko serious kidogo, sasa unakuta wakati ambapo mnaanzisha
kampuni mnakuta labda watu wa wiwili mnaleta mawazo mezani na mnapanga labda
flani afanye hivi flani afanye hivi.”
Akazama ndani kwa ufafanuzi wa kilichotokea, “kilichotokea
ni kwamba wakati wazo linatokea tulikuwa watu watano na mpaka mwendelezo wake
tulikuwa watano kwa hiyo tukaona kwamba hapa tuko kamili labda kinachotakiwa ni
mtu ambae tunaweza kumuuzia share zetu. Lakini hata Bou Nako pia ambae yuko
Nako 2 Nako, na WEUSI kama kampuni nae ni Part of it, tunapopata kazi ambazo
tunaweza kufanya nae ni mtu wa karibu.”
Hapo sawa kumbe bado Bou Nako ni part of WEUSI in one way or
another. Na kuhusu issue ambayo wengi wamekuwa wakihoji kuwa collaboration
nyingi za members wa Nako 2 Nako na River Camp soldiers hazimhusishi Bou Nako,
Warawara aliitolea ufafanuzi zaidi,
“ Bou Nako alikuwa akifanya kazi zake kama solo artist, kama
G-Nako nimekuwa nikifanya kazi zangu kama solo artist, Lord Eyez hali
kadhalika, kinachotokea ni kwamba mara nyingi tunavyotengeneza muziki unakuta
labda niko na Joh, ama wengine ambao unakuta niko nao mara nyingi, lakini Lord
eyez anafanya project zake na mimi nafanya project zangu, kwa hiyo tunafanya
kitu ambacho kinatokea at the right time right moment,” alifunguka the finest
wa A.R.
Sikiliza interview hiyo kwa kubonyeza link;- http://www.leotainmenttz.com/2012/12/g-nako-afafanua-uhusiano-wa-kampuni-ya.html
0 maoni:
Post a Comment