Pages

Thursday, December 20, 2012

Kumbe Video mpya ya Diamond 'KESHO' imevuja kimakosa!! Aelezea jinsi ilivyokuwa..

Video mpya ya Diamond 'KESHO' ambayo imeanza kuonekana kwenye mtandao wa internet  jana usiku, ilivuja kimakosa na kusambaa kwa watu. 

Diamond kupitia kipindi cha Power Jams cha East Africa Radio leo amesema kampuni ya Ogopa Djs ya nchini Kenya ambao ndio wametengeneza video hiyo waliitupia 
walii-upload video hiyo youtube kama njia ya kumtumia Diamond na uongozi wake waitazame kwanza kama iko sawa kabla ya makabidhiano rasmi.

Akaendelea kusema baada ya Diamond kutumiwa link ya video hiyo na kuitazama aligundua baadhi ya makosa na kuwaomba Ogopa warekebishe, na baadhi ya makosa ni pamoja na titles za video zinazoonyesha producer wa wimbo ni Wasafi Entertainment na huku aliefanya wimbo huo ni Marco Chali wa Mj Records.

Diamond aliendelea kufunguka kuwa baada ya kukubaliana na Ogopa waliiondoa kwenye youtube video hiyo lakini ilikuwa too late kwani tayari watu walikuwa wameishai download na kuiweka katika akaunti zao binafsi.

Diamond alimalizia kwa kusema video rasmi ya 'Kesho' itatoka rasmi Ijumaa ya wiki hii na pia bado yeye na management yake wanajadiliana kama itoke video na audio pamoja ama video peke yake.

Una maoni gani juu ya story hii? Andika maoni yako hapo chini.

0 maoni:

Post a Comment

Labels