Ni watu wengi wamehitaji kufahamu kuhusu kauli ya familia ya Marehemu
mwigizaji/msanii Sharo Milionea baada ya tangazo la Airtel lenye sauti
yake kuendelea kutumiwa na kampuni hiyo wiki kadhaa baada ya Sharo
kufariki kwa ajali ya gari iliyotokea novemba 26 2012 Tanga.
Mjomba wa Marehemu ambae ndio msemaji wa familia Shaban Mkiete
amethibitisha kwamba wamezungumza na kukubaliana na kampuni ya Airtel na
hapa namkariri akisema “ni kweli tumekubaliana, kwa mujibu wa mkataba
wao lilikua linaisha terehe 31 mwezi huu tumekubaliana kwamba liendelee
kwa makubaliano ambayo tumekubaliana nayo sisi kati ya mzee Majuto ambae
bado yupo na familia ya Marehemu, mama mzazi wa Sharo Milionea
ameridhia hilo hakuna tatizo”
Siku ya msiba millardayo.com ilipopata nafasi ya kuongea na mwakilishi
wa Airtel alisema Marehemu Sharo Milionea alifariki ndani ya kipindi cha
miezi 6 tu toka asaini dili la kuwa balozi wa Airtel na kufanya
matangazo mbalimbali yeye na mzee Majuto.
Sio tu dili la Airtel, imefahamika tayari Sharo Milionea alikua amesaini
mikataba mizuri na makampuni mbalimbali wakiwemo Wamarekani
waliotengeneza filamu maarufu Afrika kama Yellow Card, Neria na nyingine
ambapo kwa sasa Wamarekani hao wako hapa Tanzania na wametengeneza
series kadhaa ikiwemo Wahapahapa na Siri ya Mtungi ambayo ndio Sharo
Milionea kashiriki ndani na mpaka anafariki tayari alikua ameshaanza
kucheza igizo hilo.
0 maoni:
Post a Comment