Pages

Sunday, December 16, 2012

CHECK OUT NA MAANDALIZI YA MISS UTALII TANZANIA 2012/2013 YATAKAO FANYIKA HIVI KARIBUNI.

 VIONGOZI WA BARAZA LA SANAA LA TAIFA (BASATA) WAKIWA KATIKA MKUTANO WA  MAANDALIZI YA FAINALI ZA TAIFA ZA MISS UTALII TANZANIA  NA BODI  YA MISS UTALII TANZANIA 2012/2013 ZITAKAZO FANYIKA HIVI KARIBUNI.
 BODI  YA MISS UTALII TANZANIA WAKIWA KATIKA KIKAO CHA PAMOJA NA VIONGOZI WA BARAZA LA UTAMADUNI TANZANIA (BASATA)  WAKIENDELEA NA KIKAO.
WAJUMBE  WA BODI YA MISS UTALII TANZANIA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI WA BARAZA LA SANAA TAIFA (BASATA) BAADA YA KIKAO CHA MAANDALIZI YA FAINALI HIZO ZA MISS UTALII 2012/2013.

*************************************************************************
Wakati kambi ya Miss Utalii Tanzania 2012/2013 ikikaribia kuanza katika Hotel ya Ikondolelo Jijini Dar es salaam, juzi tarehe 14.12.2012 Bodi ya Taifa ya mashindano hayo ilifanya kikao na Serikari kupitia Baraza la Sanaa la Taifa katika ukumbi wa Baraza hilo. 
Katika kikao hicho ambacho  kilijadili maandalizi ya fainali na mpango mkakati wa fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu.

Katika kikao hicho Bodi ya Miss Utalii Tanzania iliwasilisha taarifa ya kukamilika kwa maandalizi kwa Serikali ambapo bodi iliitaarifu Serikali kuwa maandalizi ya fainali hizo yamekamilika kwa asilimia tisini 90% ikiwemo katika maeneo ya kambi na mafunzo, ukumbi, Zawadi, wadhamini,Washiriki, Nk.

Bodi ilibainisha kuwa kwamba jumla ya washiriki sitini (60) wakiwakilisha mikoa yote ya Tanzania na Kanda maalum za vyuo vikuu  watapanda jukwaani kuwania taji la Miss Utalii Tanzania 2012/2013. 
Pia Bodi ilibainisha kuwa zawadi zitakazo tolewa kwa washindi zimelenga zaidi kuwanufaisha washiriki , jamii zao na taifa. 
Zawadi hizo ni pamoja na Nafasi za masomo za elimu ya juu, mikataba ya kazi ,Safari za kushiriki mashindano ya Dunia na Kimataifa , Tuzo za heshima za kijamii, kitalii, kitamaduni, urembo na mitindo.

Aidha Bodi ilielezea kuwa imejipanga kuzifanya fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/2013 kuwa tukio kubwa la pekee Kihistoria na kitamaduni kuwahi kufanyika nchini kabla na baada ya uhuru.  
Ambapo wakiwa kambini washiriki watafanya shughuli mbalimbali za kijamii pamoja na kupata mafunzo stadi mbalimbali za maisha , uhamasishaji na utangazaji wa elimu , utalii, utamaduni, uwekezaji,mazingira, michezo na afya.

Nayo Serikali ilipongeza Bodi ya maandilizi ya miss utalii Tanzania kwa mpango mkakati na maandalizi yenye kukidhi na kulenga kupromoti utalii uhamasishaji na utangazaji wa elimu , utamaduni, uwekezaji,mazingira, michezo na afya.
Akizungumza katika mkutano huo Kaimu Katibu mtendaji wa Baraza la sanaa la Taifda Ndugu. 
Malimi Mashili alipongeza mpangilio wa zawadi na tuzo kwa washindi pamoja na washiriki ambapo tofauti na mashindano mengine ambapo zawadi zao huwa ni mzigo kwa washiriki na wakati mwingine zisizo na manufaa kwa jamii wala  Taifa.
"Miss utalii Tanzania katika kipindi cha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake  imekuwa ni fahari ya Taifa na kielelezo cha utamaduni wa Tanzania kitaifa na kimafaifa ambapo limekuwa ndilo shindano pekee linalo la tangaza nchi yetu kwa kushinda mataji ya Dunia na kimataifa kila mnapo shiriki". 
Aidha akiahirisha mkutano huo aliihakikishia Bodi kuwa Serikali inatambua juhudi na mchango wa waandaaji na mashindano ya miss utalii tanzania katika kukuza utalii, utamaduni na michezo nchini na kwamba Serikali  sikuzote ipo bega kwa bega na waandaaji wa mashindano haya katika kuhakikisha kwamba hayakwami na iko tayari kusaidia kwa hali na mali  ili yaweze kufanyika kwa kiwango cha kimataifa.

Imetolewa na,
Mratibu Matukio,
Hamis .A. Mkongowale

0 maoni:

Post a Comment

Labels