Pages

Tuesday, December 04, 2012

DULLY SYKES ATIMIZA MIAKA 32, AJA NA 'UTAMU UTAMU' KWA ZAWADI KWA MASHABIKI WAKE




MSANII mwenye jina Kubwa katika tasinia ya muziki wa kizazi kipya Tanzania Dully Sykes amewapa mashabiki wake zawadi ikiwa ni moja ya maadhimisho ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo  ametimiza miaka 32

Ametoa zawadi ya 'single' yake mpya inayokwenda kwa jina la Utamu Utamu akiwa amewashirikisha wasanii wenzake wa bongo fleva wanaotikisa kwenye anga za muziki Diamond, pamoja na Omy Dimpozi
 Dully alisema kuwa katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ameamua kuwaweka karibu zaidi mashabiki wake kwa kumalizia kuitengeneza video yake ya Utamu Utamu ambapo hivi karibuni ataizindua ikiwa ni zawadi kwao

"Nimetimiza miaka 32 nashukuru mungu lakini sifikirii kufanya part yoyote ile kwani sitaki kuwa na mkusanyiko wa watu wachache ila ninachokiwaza ni kutoa zawadi kwa mashabiki na wadau wote kama shukurani kwa siku ya kuzaliwa kwangu" alisema Dully

Alisema kuwa single hiyo itakuwa bomba na kufanya vizuri kwa sababu na maaandalizi yaliyoandaliwa kwa ajili ya kuiboresha video hiyo

"Wasanii nilishorikiana nao ni wakali na wanatikisa katika anga za muziki hivyo kila kitu kitakuwa vizuri na ngoma itafanya vizuri sana naamini hivyo, kwani siajawahi kuwaangusha mashabiki wangu tangu nimeanza muziki" alisema

0 maoni:

Post a Comment

Labels