Pages

Monday, December 03, 2012

RAPPER LORD EYEZ ATUNGA MISTARI KAMA UJUMBE KWA RAY C


 
Rapa maarufu nchini Tanzania Isack Waziri 'Lord Eyez amefunguka kuwa ametunga mistari michache ya Wimbo kama ujumbe wake kwa msanii Rehema Chalamila maarufu kama Ray C ambawo hapo awali waliwahi kuwa wapenzi na kuripotiwa kuwa mbioni kufunga ndoa kabla wawili hao kuachana

Akizungumza katika mahojiano yake na kituo cha televisheni  jijini Dar es Salaam alisema kuwa ameamua kutunga mistari kuhusiana na matatizo yanayomkabili kwa sasa kwa lengo la kumfariji msanii huyo

Alisema kuwa anasikitika na baadhi ya watu kumuhusisha katika matatizo yanayomkabili Ray C yanayotokana na matumizi ya madawa ya kulevya jambo ambalo anadai hausiki nalo

"Sihusiki kabisa na swala la Ray C kutumia dawa za kulevya na naomba watu wasiniongeze mzigo kwa kunihukumu katika vitu ambavyo sihusiki navyo, hata mimi tatizo lake limenigusa na ninamuombea sana arudi katika hali yake ya kawaida na ninaamini mungu atamsaidia na atakuwa pouwa " alisema Lord Eyez

0 maoni:

Post a Comment

Labels